- 218 viewsDuration: 47sGavana wa Kakamega, Fernandes Barasa, ametangaza kuwa zahanati sasa zitaruhusiwa kutoa huduma za uzazi chini ya bima ya Afya ya Jamii, SHA. Akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya Chuo cha Matibabu cha FAFA huko Matungu, Barasa alisema hatua hiyo itaongeza upatikanaji wa huduma muhimu za afya karibu na wananchi.