- 2,321 viewsDuration: 4:32Wiki mbili zilizopita, Rais William Ruto aliamuru wanafunzi wote wa Gredi ya 10 ambao hawakuwa wameripoti shuleni kufika shuleni mara moja, iwe hawana karo, sare za shule au mahitaji mengine. Akitoa agizo hilo, rais aliwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa serikali ingegaramia malipo yoyote. Hata hivyo wazazi na wanafunzi kutoka baadhi ya mitaa jijini nairobi waliofuata agizo hilo, wanaelezea kuwa walimu wakuu shuleni walidinda kuwapa nafasi, huku wakisema serikali haikutoa hela za kufadhili ahadi hiyo.