- 237 viewsDuration: 4:14Licha ya kuongoza waumini katika ibada na maombi kanisani huko mwiki, Agnes Nyambura Wainaina amekuwa mkombozi wa wazee haswa waliotelekezwa na jamaa zao katika mtaa wa dandora hapa Nairobi. Ni shughuli anayoifanya kwa takriban miaka minne sasa huku wazee hao wakipata matumaini ya kuishi nyema kila siku kupitia huduma anazowapa kama vile matibabu, chakula na hata kuwalipia kodi ya nyumba baadhi yao. Inayofuta ni simulizi yake kwa kina huku tukimvisha taji la mwanamke bomba wiki hii.