- 465 viewsDuration: 3:08Akina mama kumi waligunduliwa kuwa na saratani ya mlango wa uzazi ndani ya saa nne za zoezi la upimaji lililofanyika katika Kaunti ya Samburu. Takwimu hizo za kushtua zilibainika katika kambi ya matibabu eneo hilo ambapo wakazi walifika kufanyiwa vipimo vya saratani. Na kama anavyoarifu mwanahabari wetu Bonface Barasa, wakazi wametakiwa kujitokeza mapema kupimwa ili kujua hali yao na kufanikisha matibabu ya ugonjwa huo sugu.