Aliyekuwa waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiangi afika katika makao makuu ya DCI

  • | Citizen TV
    1,350 views

    Aliyekuwa waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiangi amefika katika makao makuu ya upelelezi wa jinai DCI, kama alivyohitajika. Matiang'i alifika katika makao hayo mwendo wa saa tatu asubuhi, ambapo alizuliwa kwa muda kwenye lango kuu. Maafisa wa DCI walitaka kujua idadi kamili ya mawakili aliokuwa nao na walikuwa kina nani. Baadaye waziri huyo wa zamani aliruhusiwa kuingia na kwa sasa anaendelea kuhojiwa kuhusiana na uvamizi aliodai ulifanyika kwake nyumbani mwezi jana.