Asilimia kubwa ya wakazi kutoka Mlima Kenya wanasema Gachagua amefanya kazi

  • | Citizen TV
    2,561 views

    Utafiti wa kampuni ya TIFA umebaini kuwa wakenya wana maoni kinzani kuhusu utendakazi wa naibu rais rigathi gachagua. Asilimia kubwa ya wanaosema amefanya kazi nzuri ni wakazi wa eneo la Mlima Kenya ambapo asilimia 59 wanamsifia ikilinganishwa na asilimia 27 ya wananchi kutoka maeneo mengine. Aidha asilimia 28 ya wakazi wa mlima kenya wanasema hajawajibika ikilinganishwa na asilimia 11 ya wakazi wengine.