Askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana Jackson Ole Sapit awaonya wanasiasa dhidi ya maneno ya chuki

  • | Citizen TV
    211 views

    Askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana Jackson Ole Sapit amewarai viongozi wa mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio la umoja kukoma kutoa matamshi yanayoweza kuvuruga mazungumzo ya upatanisho yanayoendelea ili kutatua masuala yanayokumba nchi hii. Ole Sapit amesema viongozi wa makanisa wanaunga mkono mazungumzo ya Bomas kwani ndio njia pekee ya kuhakikisha utulivu unaohitajika. Ole Sapit amesema haya katika hafla ya kupokezwa kwa kanisa la kianglikana na shule kutoka mfanyibiashara David Langat katika eneo Lol-kireng', Nandi Hills kaunti ya Nandi.