Skip to main content
Skip to main content

Askofu wa dayosisi ya Kapsabet John Lelei awataka wanasiasa kuheshimiana wanapopiga siasa

  • | Citizen TV
    180 views
    Askofu wa Dayosisi ya kanisa katoliki ya Kapsabet John Lelei amewataka viongozi wa kisiasa nchini kuwa watulivu na kuheshimiana wanapotekeleza shughuli zao za kisiasa. Akizungumza mjini Kapsabet, Askofu Lelei alishutumu matumizi ya makundi ya wahuni kuvuruga mikutano ya kisiasa au kuzua taharuki miongoni mwa viongozi na wananchi. Askofu huyo amesema siasa zinapasa kufanywa kwa njia ya amani na heshima huku viongozi wakipeperusha sera na ajenda zao bila kutumia lugha za matusi, vitisho au propaganda dhidi ya wapinzani wao. Askofu huyo alieleza kuwa viongozi wana wajibu wa kuwaleta pamoja wananchi badala ya kuwagawa kupitia matamshi ya uchochezi ambayo yanaweza kuhatarisha mshikamano wa kitaifa.