Baadhi ya wanafunzi hawajaingia kidato cha kwanza

  • | Citizen TV
    293 views

    Ni wiki ya tatu sasa baada ya wanafunzi waliomaliza mtihani wa KCPE kuripoti shuleni. Japo kuna wale ambao hawajafika shuleni na serikali kuanzisha kampeni ya kuhakikisha wote wanajiunga na shule za upili, idadi hii katika eneo la kati imefikia asilimia 95 kukiwa na zaidi ya wanafunzi 4000 ambao bado hawajafika shuleni kuendelea na masomo yao katika kaunti tano za eneo hilo. Tunaungana na Martin Munene Moja kwa Moja akiwa katika kaunti ya Nyeri kwa maelezo zaidi