- 593 viewsDuration: 1:33Baraza la wazee wa jamii ya Waluo lawakosoa viongozi wa kisiasa kutokana na vurugu zilizoshuhudiwa jijini Kisumu. Naibu mwenyekiti wa baraza hilo James Ayaga asema kuwa vurugu hizo hazingetokea iwapo viongozi wangekuwa na hekima na kufuata sheria zilizoko iwapo wangehitaji usalama. Hii ni baada ya asasi za usalama kubaini kuwa makundi hayo mawili ya wahuni waliokabiliana nje ya kanisa la St. Stephen’s wafadhiliwa na wanasisasa. Vurugu hizo zasababisha vifo vya watu wawili na pikipiki tisa kuteketezwa .