Skip to main content
Skip to main content

Bastola ya Jaji Muchelule yapatikana kwa mshukiwa wa ujambazi

  • | Citizen TV
    18,557 views
    Duration: 2:22
    Polisi wanachunguza tukio ambapo bastola ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa Aggrey Muchelule ilipatikana nyumbani kwa mshukiwa wa ujambazi aliyeuawa kwa kupigwa risasi. Mshukiwa huyo alihusishwa na tukio la ujambazi lililotokea hivi majuzi katika mkahawa mmoja eneo la Westlands. Jaji Muchelule ameandikisha taarifa kwa polisi akisema mara ya mwisho alikuwa na bastola hiyo mwaka jana, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ilivyofika mikononi mwa mshukiwa.