- 6,847 viewsDuration: 1:37BBC imefichua matokeo ya ripoti rasmi kuhusu sababu za ndege ya mafunzo ya Jeshi la Anga la Bangladesh kuanguka katika shule iliyokuwa na wanafunzi. Uchunguzi umebaini kuwa rubani aliendesha ndege kwa namna ambayo ilisababisha injini ya ndege kupoteza nguvu lakini huenda ndege iligongana na ndege wa porini kabla ya rubani kubadilisha mwinuko wa safari jambo ambalo linaweza kuwa lilisababisha tatizo la kiufundi. Takribani watu 36, wengi wao wakiwa watoto, waliuawa wakati ndege hiyo ilipogonga Shule na Chuo cha Milestone mwezi Julai 2025. #bbcswahili #bangladesh #ajaliyandege Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw