Biashara na barabara zafungwa kufuatia maandamano Migori

  • | Citizen TV
    5,940 views

    Uchukuzi umetatizika na biashara nyingi kufungwa baada ya wafuasi wa Azimio la umoja one kenya alliance kufanya maandamano mjini Migori. Waandamanaji hao walifunga barabara kuu ya Migori kuelekea Isebania na kuwalazimu waendeshaji magari kutafuta njia mbadala. Waandamanaji hao wanalalamikia gharama ya juu ya maisha, na kuitaka serikali kushughulikia bei ya bidhaa muhimu. Aidha maandamano hayo yanajiri kufuatia wito wa viongozi wa Azimio kuwataka wakenya wakenya kumimikina barabarari kuwajibisha serikali kuhusu masuala kadhaa haswa gharama ya juu ya maisha na kufunguliwa kwa sava za IEBC. Aidha maandamano kama hayo yalifanyika katika kaunti ya Nyandarua, na kuongozwa na mshirikishi w aazimio eneo hilo Dickosn Manyara.