Bunduki tano na risasi 14 zimesalimishwa katika eneo la Trans Mara, kaunti ya Narok, huku serikali ikiendelea kuimarisha juhudi za kurejesha amani kufuatia mapigano ya hivi maajuzi yaliyosababisha vifo vya watu wanne na kuwafanya wengine 1,800 kuhama makazi yao. Waziri wa Usalama wa Taifa, Kipchumba Murkomen, pia ametangaza kipindi cha siku saba cha msamaha kwa raia wanaomiliki silaha kinyume cha sheria katika eneo hilo kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa operesheni ya kuzitwaa silaha hizo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive