- 18,745 viewsDuration: 1:39Bunge la Ulaya linatarajiwa kujadili ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini Tanzania, mauaji ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, pamoja na kuendelea kuzuiliwa kwa kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Pendekezo lililo mbele ya bunge hilo linataka Tume ya Bara Ulaya kusitisha misaada ya moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania, kutoa msaada kwa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na wanahabari, na pia linapendekeza vikwazo dhidi ya watu waliohusika katika ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini Tanzani. #DiraYaDuniaTV