CCTV yanasa mtu anayeaminika kuhusika na mauaji ya marehemu Charles Ong'ondo Were

  • | Citizen TV
    6,633 views

    Uchunguzi wa mauaji ya mbunge wa Kasipul Charles Ong'ondo Were umeendelea huku maafisa wa upelelezi sasa wakipata picha ya mtu anayeaminika kuhusika na mauaji ya marehemu. Picha za CCTV zilimnasa mshukiwa akimpigia darubini mheshimiwa Were akiwa kwenye barabara ya Wabera katikati ya jijini la Nairobi. Mshukiwa huyu pia akinakiliwa kwenye picha za CCTV karibu na eneo ambako mbunge huyo alipigiwa risasi. Franklin Wallah anatufungulia Nipashe jioni ya leo