Chama cha 'Equatable Party' chataka ushuru wa haki kwenye bajeti

  • | Citizen TV
    74 views

    Chama cha The Equatable Party (TEP) kimependekeza kushukishwa kwa ushuru unaotozwa wafanyabiashara ili kutoa nafasi kwa wawekezaji wengi na biashara kunawiri. akizungumza wakati wa kuzindua usajili wa wananchama katika kaunti ya Kwale, kinara wa chama hicho Gilbert Shanga amesema hatua hiyo itawezesha biashara nyingi kutoa nafasi zaidi za ajira kwa wakenya. Aidha chama hicho kimetaka mgao wa basari kuondolewa kutoka kwa viongozi wa kisiasa na mgao huo kupelekwa moja kwa moja kwa shule zote za umma kulingana na mahitaji ya shule hizo.