Skip to main content
Skip to main content

Chama cha Komrades kimefaidi kina mama kiambu huku Elizabeth akiongoza kikundi kufaulu

  • | Citizen TV
    1,128 views
    Duration: 6:53
    Mwaka unapoanza ni kawaida watu hujiwekea malengo ya maendeleo huku wanawake wengi wakichukua fursa hiyo kuanza vyama vya kuwekeza pesa kwa nia ya kusaidiana na kuinuana kifedha. Hata hivyo asilimia kubwa ya vyama hivyo havifiki mbali wala kutimiza malengo kutokana na sababu mbali mbali. Lakini mambo ni tofauti kwa kikundi kimoja kinachojulikana kama komrades ambacho kinajivunia maendeleo chungu nzima huku kikimpa sifa mwanzilishi wake Elizabeth kwa usimamizi bora. Je ndoto ya Elizabeth ilianzia wapi na ni kipi haswa kinachomfanya awe tofauti na viongozi wengine? Hebu tusikilize simulizi yake katika makala yetu ya kwanza ya mwanamke Bomba mwaka huu.