Chama cha madaktari nchini KMA chashutumu wizi wa fedha katika NHIF

  • | Citizen TV
    165 views

    Chama cha madaktari nchini KMA kimeshutumu ripoti za wizi wa fedha katika malipo ya bima ya matibabu nchini ya NHIF. Kwenye taarifa, katibu mkuu wa KMA daktari Diana Marion amesema kuwa wameghadhabishwa na ripoti za baadhi ya hospitali kushirikiana na NHIF kuwaibia wakenya. Chama hiki sasa kikisema kitashirikiana na bodi ya madaktari na wahudumu wa afya KMPDC kuendesha uchunguzi, na madaktari watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua. Taarifa hii aidha imetaka ulinzi kutolewa kwa watu wanaotoa ripoti za ufisadi katika sekta ya afya.