- 74,909 viewsDuration: 28sTazama chui huyu aliyegongwa na gari kwenye barabara kuu kusini-magharibi mwa India alivyomjeruhi mmoja wa watu waliokuwa katika operesheni ya kumwondoa eneo la ajali. Ingawa alikuwa ametulizwa kwa dawa ya usingizi kupitia sindano maalumu, chui alimshambulia mtu huyo walipokuwa wakijaribu kumpakia kwenye lori. Hata hivyo, chui na mfanyakazi aliyejeruhiwa wote wako katika hali nzuri, huku maafisa wakisema kwamba mnyama huyo huenda akapelekwa kwenye kituo cha uokoaji kwa matunzo zaidi. #bbcswahili #india #wanyama Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw