- 277 viewsDuration: 1:34Wakazi wa Kobujoi katika kaunti ya Nandi walinunua ng'ombe wa maziwa na kuwapeleka katika Chuo Kikuu cha Kaimosi bewa la Kobujoi kama ishara ya shukrani baada ya kuanzishwa kwa bewa la chuo hicho eneo hilo. Kulingana nao chuo hicho, kitaleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwapa vijana wa eneo hilo fursa ya kupata elimu ya juu karibu na nyumbani. Wakazi hao wameitaka serikali kuendelea kuwekeza zaidi katika miundombinu ya chuo hicho ili kuhakikisha kinatoa huduma bora za elimu