Chuo kikuu cha Maasai Mara kimeanzisha mashindano ya riadha kwa lengo la kukuza utalii na kupambana na mabadiliko ya tabianchi eneo hilo.
Mashindano hayo yalijumuisha mbio za kilomita 10, kilomita 6, kilomita 4 na kilomita 2 kwa makundi mbalimbali. Hillary kibet ndiye aliyekuwa bingwa wa mbio za kwanza za Maasai Mara run baada ya kuwashinda John Kareithi na Victor Chepkwony waliomaliza katika nafasi ya pili na ya tatu mtawalia katika mbio za kilomita 10 kwa wanaume. Katika mbio hizo kwa wanawake, Fancy Chepkoech aliwashinda Damaris Towet na Faith Chelang’at na kutwaa ushindi.