COTU yataka TSC iwajibike na kutatua mgomo wa KUPPET

  • | Citizen TV
    1,149 views

    Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini (COTU) umeitaka Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kushirikiana na Muungano wa Walimu wa shule za upili (KUPPET) kufanya makubaliano ya kurejea kazini. Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli amesisitiza kuwa makubaliano hayo ni muhimu kwa sababu serikali imekubali kutimiza baadhi ya matakwa ya KUPPET. Atwoli pia alikashifu Tume ya Kuajiri Walimu kwa kukimbilia mahakama na kuzuia KUPPET kuendeleza mgomo huo, akisema kuwa agizo hilo limepitwa na wakati.