- 12,287 viewsDuration: 2:42Kitengo cha uchunguzi wa jinai na wataalam wa maswala ya upelelezi wameanzisha uchunguzi wa kifo cha mbunge wa zamani wa Lugari Cyrus Jirongo. Tayari polisi hao wamepata picha za CCTV kutoka kwa kituo cha petroli eneo kulikotokea ajali, pamoja ma taarifa za mashahidi muhimu kwenye uchunguzi. Kumekuwa na maswali kuhusu haswa kilichojiri baada ya jirongo kuondoka eneo la karen hapa nairobi na kisha kupatikana kwenye ajali ya barabarani eneo la naivasha kaunti ya Nakuru.