- 10,460 viewsDuration: 2:55Wapelelezi wanaochunguza kifo cha aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Lugari, Cyrus Jirongo, wamefanikiwa kuwatafuta na kuwahoji watu wanaohusishwa na gari lililonakiliwa na kamera za CCTV karibu na eneo la ajali ya barabarani iliyotokea Karai, Naivasha, ambapo Jirongo alipoteza maisha yake. Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), makachero walifika Keringet,Kuresoi Kusini, Kaunti ya Nakuru, na kunakili maelezo kutoka kwa watu wanaohusishwa na gari aina ya Toyota Probox jeupe lenye nambari ya usajili KDJ 564E. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive