Skip to main content
Skip to main content

Duale asema serikali haitasitisha ujenzi wa karantini ya Ebola Laikipia

  • | Citizen TV
    932 views
    Duration: 3:41
    Waziri wa Afya Aden Duale sasa anasema serikali haitasitisha ujenzi wa karantini ya Ebola ya Wamarekani ndani ya kambi ya kijeshi ya Laikipia. Akitoa taarifa bungeni, Duale amesema kuwa kituo hicho ni mojawapo ya vituo 23 ambavyo serikali inajenga kote nchini kwa maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari. Duale alikabiliwa na pingamizi kali kutoka kwa wabunge waliotaka kuelewa sababu ya wagonjwa wa Ebola wa Wamarekani kutopelekwa kwingineko na badala yake kuletwa nchini kutibiwa.