Familia moja katika eneo la Bibirioni, kaunti ya Kiambu inatoa wito wa msaada wa kifedha wa shilingi Milioni-4.5 zitakazofanikisha upandikizaji wa figo wa mpendwa wao. Jonathan Kimani Waroja, mwenye umri wa miaka-21, aligunduliwa kuwa na matatizo ya figo mwaka-2024, hali ambayo baadaye ilidorora na kusababisha figo yake kukosa kufanya kazi mwezi Disemba mwaka uliopita. Ni hali ambayo imempa mahangaiko tele kwani anategemea matibabu ya usafishaji damu mara mbili kila wiki ili aweze kuishi. Madaktari wamemshauri kufanyiwa matibabu hayo ya dharura kama suluhu ya kudumu kwa hali yake.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive