Skip to main content
Skip to main content

Familia moja kijijini Lugulu yaomboleza vifo vya jamaa watatu kutokana na ajali

  • | Citizen TV
    1,268 views
    Duration: 1:42
    Familia moja kijijini Lugulu katika eneo bunge la Butula kaunti ya Busia inaomboleza vifo vya jamaa wao watatu waliofariki kutokana na ajali ya barabarani kwenye barabara ya Butula-Bumala eneo la Bar-Ober. Ajali hiyo ilifanyika baada ya gari walimokua wameabiri kubingiria mara kadhaa barabarani, watu sita wakinusurika kifo na kupata majeraha wakitoka kuhudumu katika hafla ya matanga. Watatu hawa ni familia moja kijijini lugulu na walikuwa wakitoa huduma za chakula matangani. Familia hiyo inadai vifo vya lilian na margaret vilichangiwa na utepetevu katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya busia kwa kukosekana kwa huduma za dharura.