- 784 viewsDuration: 3:36Familia ya Kevin Maseri, aliyepigwa risasi na kuuwawa katika mtaa wa kitengela siku 11 zilizopita imelalamikia kucheleweshwa kwa kesi hiyo, wakimtaka mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Renson Ingonga kufanya hima na kuhakikisha washukiwa wamefikishwa mahakamani. Wakizungumza wakati wa mazishi yake katika kijiji cha matali, familia ya jamaa huyo na viongozi pia wamemtaka inspekta jenerali wa polisi douglas kanja kuwasimamisha kazi maafisa wa polisi wanaohusishwa na mauaji hayo