- 4,015 viewsDuration: 2:50Familia moja eneo la Kitutu Chache kaunti ya Kisii sasa inataka serikali kuingilia kati kumuokoa jamaa yao aliyekwama nchini Saudi Arabia kufuatia mgogoro wa uajiri. Familia hii inadai kuwa, kijana wao mwenye umri wa miaka 33 amefungiwa kwa mwezi wa tatu sasa na mwajiri wake wa zamani mjini Riyadh baada ya kutaka kuhamia kwa mwajiri mwingine. Familia ya kijana huyo Justin Mogendi imesema imetakiwa kulipa shilingi laki nane jamaa yao kuachiliwa