Skip to main content
Skip to main content

Fifa yapinga kusimamishwa kwa rais wa FKF

  • | Citizen TV
    357 views
    Shirikisho la Soka Duniani FIFA limepinga kusimamishwa kazi kwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini FKF Hussein Mohamed, likisema kuwa taratibu zilizotumiwa na wanachama tisa wa Kamati ya Kitaifa NEC kumtimua zilikuwa na makosa. Katika taarifa yake, FIFA imesema kuwa ombi lililotolewa la kubaini iwapo hatua zilizochukuliwa zilizingatia katiba ya FKF halikuafikiwa. Aidha, imesema nyaraka zilizowasilishwa na NEC hazionyeshi kuwa taratibu sahihi zilifuatwa, hivyo kukataa mchakato huo. FIFA imeongeza kuwa haitambui maamuzi yaliyofanywa na baadhi ya wanachama wa NEC ambayo hayakufuata ipasavyo Kifungu cha 41 cha Katiba ya FKF, ambacho kinataka kuheshimiwa kwa taratibu za nidhamu na kuhakikisha maafisa wanaohusishwa wanasikilizwa kwa haki.