- 14,611 viewsDuration: 4:07Kinara wa Chama cha DCP Rigathi Gachagua sasa anasema kuwa hana nia ya kushinikiza kuvunjwa kwa vyama vingine vya kisiasa katika eneo la Mlima, ila tu hatafanya mazungumzo ya muungano na vyama ambavyo havijaimarisha ngome zao za kisiasa. Akizungumza nyumbani kwake Wamunyoro baada ya mkutano na vinara wa vyama vya DP, PNU na DEP, Gachagua amepuuzilia mbali madai kuwa amekuwa akikandamiza na kudunisha vyama vingine vya kisiasa kwenye upinzani, akisema kuwa vyama hivyo vimekosa umaarufu kwa sababu viongozi wake hawatii bidii kujinadi kwenye ngome zao kwanza. Gachagua pia amesema kuwa chama chake cha DCP hakipo tayari kwa mazungumzo ya kuunda muungano mpya wa upinzani kwa sasa.