- 315 viewsDuration: 1:47Gavana wa Turkana, Jeremiah Lomorukai, alikabiliwa na maswali mazito kutoka kwa Kamati ya Bunge ya Ukaguzi wa Matumizi ya pesa za Umma, inayoongozwa na Seneta Moses Kajwang, kuhusu miradi ya mamilioni ya pesa iliyokwama. Makazi ya gavana yaliyoigharimu kaunti zaidi ya shilingi milioni 200 hayajakamilika, huku jengo la makao makuu ya kaunti likisuasua kwa miaka minane licha ya vifaa vya gharama kubwa kununuliwa kabla ya miundombinu kukamilika.