Gavana Kawira Mwangaza mashakani tena

  • | Citizen TV
    8,548 views

    Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amejipata mashakani kufuatia madai ya wizi wa fedha za umma. Fedha hizi zinasemekana kuwa malipo kwa jamaa zake na washirika wa karibu. Kesi imewasilishwa katika bunge la seneti na pia kwa tume ya kupambana na ufisadi kuhusu jinsi shilingi milioni 42.4 zilivyotolewa kama malipo kwa akaunti za watu binafsi katika muda wa chini ya mwaka mmoja.