- 110 viewsDuration: 1:38Ni afueni kwa vijana kaunti ya Taita Taveta baada ya gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime kutia sahihi mswaada wa vijana wa mwaka 2025 na kuwa sheria. Katika sera hiyo serikali ya kaunti itaunda kikosi maalum cha vijana ambao watatoa huduma mbalimbali kwa jamii ikiwemo kusafisha miji ya kaunti hiyo. Kadhalika sera hiyo inatoa mwongozo wa kubuni nafasi za ajira kwa mamia ya vijana na hivyo kujiepusha na matumizi ya mihadarati na maovu mengine katika jamii.