Kaunti ya Bomet imemulikwa kwa madai ya ubadhirifu wa fedha, ulipaji haramu wa marupurupu kwa wafanyakazi na kuwalipa walimu wa chekechea mishahara duni. Gavana wa gatuzi hilo Profesa Hillary Barchok alikuwa na wakati mgumu kuelezea dosari kadhaa zilizoshuhudiwa katika ufafanuzi wa taarifa za kifedha na visa vya udanganyifu katika usimamizi wa wafanyakazi jinsi ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu wa fedha za serikali. Licha ya ripoti ya mkaguzi mkuu wa fedha za serikali kusema hitilafu hizo haziashirii kupotea kwa fedha, maseneta wana hofu kuhusiana na nia ya maafisa wa kaunti hiyo ya kuwasilisha taarifa zisizo sahihi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive