- 329 viewsDuration: 1:23Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti amewafuta kazi maafisa 36 wa kaunti hiyo kwa tuhuma za ufisadi. Akizungumza katika ofisi za kaunti hiyo mjini Machakos, gavana Wavinya amesema kwamba maafisa hao wakiwemo wa idara za usimamizi, biashara, vileo, utoaji wa bili na ukusanyaji ushuru , wamekuwa wakitoa risiti feki na hata kutoeleza kiwango kamili cha pesa zilizokusanywa. Kulingana naye, majina ya watuhumiwa yameshapelekwa kwa idara ya upelelezi kwa uchunguzi zaidi na kufunguliwa mashtaka.