Skip to main content
Skip to main content

Gavana wa Murang’a atakiwa kufafanua matumizi ya fedha kwenye kaunti

  • | KBC Video
    308 views
    Duration: 2:58
    Gavana wa kaunti ya Murang’a Irungu Kang’ata alikuwa na wakati mgumu kuelezea masuala ya ukaguzi wa matumizi ya pesa katika kaunti hiyo alipofika mbele ya kamati ya bunge la seneti kuhusu uwekezaji wa umma. Kang’ata aliyetii mwaliko wa kamati hiyo hivi leo, alitakiwa kujibu masuala kadhaa yaliyoibuliwa na ripoti ya mkaguzi mkuu wa matumizi ya pesa za umma ambaye ikiwa ni pamoja na usimamizi mbaya wa mali ya kaunti, taarifa kinzani kuhusu mapato, vyumba vya upasuaji hospitalini visivyotumika na ukosefu wa hati miliki za ardhi ya hospitali. Akijitetea, kang’ata alilaumu kucheleweshwa kwa mgao wa fedha kutoka halmashauri ya afya ya jamii SHA, akisema kunaathiri utoaji huduma. Abdiaziz Hashim na maelezo zaidi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive