- 870 viewsDuration: 3:06Kuwekeza jijini Nairobi ni manufaa makubwa kwa Umoja wa Mataifa. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa shirika hilo António Guterres, ambaye amezindua ujenzi wa ukumbi wa kongamano na ofisi zaidi za Umoja wa Mataifa katika makao ya Gigiri jijini Nairobi. Guterres amesema kwamba ujenzi wa ofisi hizo utakuwa na manufaa makubwa kwa Wakenya, huku pia wafanyakazi zaidi wa Umoja wa Mataifa wakitarajiwa nchini mwaka huu kutoka jijini New York.