- 2,790 viewsDuration: 4:35Hebu tafakari haya: umefanya mtihani wa gredi ya tisa, KJSEA, kisha ukasalia kusubiri matokeo ambayo hadi sasa hayajatolewa kwasababu hata hukufanya mtihani unaodhania kuwa ulifanya. Ilikuwa ni hadaa tu ya usimamizi wa shule na maafisa wa elimu wa kaunti. Hii ndio hali ambayo amejipata kwayo msichana mmoja huko nyamira ambaye alifanya mtihani feki wa kjsea na sasa yuko kwenye njia panda akikosa kuteuliwa kwa shule ya sekondari ya juu kwasababu hana matokeo ya gredi ya tisa