Hali ya taharuki yaendelea kutanda kaunti ya Samburu kwa sababu ya uhalifu

  • | Citizen TV
    384 views

    Hali ya taharuki bado imetanda katika kaunti ya Samburu, hali ambayo inafanya familia nyingi kutoroka makazi yao wakitafuta usalama. Aliyekuwa mwakilishi wa kike kaunti ya Samburu Maison Leshoomo amesema kuwa maeneo ya Posta, Longewan, Lolmolog na Pora yamekuwa hatari kwa usalama huku shughuli za masomo zikiendelea kusambaratika. Leshoomo amewaomba viongozi haswa wazee wa kutoka pande zote za Pokot na Samburu kuketi pamoja na kutafuta suluhu ya mashambulizi ya mara kwa mara. Leshoomo amewarai viongozi kutoka kaunti ya Samburu kutotoa matamshi ambayo yanaweza kuleta chuki au wasiwasi