- 438 viewsDuration: 59sTimu ya taifa ya kandanda ya kina dada, Harambee Starlets, inatarajiwa kusafiri usiku wa leo kuelekea Miramas, Ufaransa, baada ya kupokea malipo yao kutoka Wizara ya Michezo. Wachezaji hao walikuwa wameandamana hadi makao makuu ya Football Kenya Federation wakidai malipo yao kabla ya safari. Katibu katika Idara ya Michezo, Elijah Mwangi, aliingilia kati na kukabidhi timu hiyo shilingi milioni 10 zilizoahidiwa na Rais William Ruto wakati wa mkutano na wachezaji hao jana.