Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, inaendelea na maandalizi jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini kuelekea mchuano wa kwanza wa kufuzu kwa fainali za AFCON 2027 dhidi ya wenyeji Bafana Bafana.
Kikosi hicho kilichotua Johannesburg Jumanne, kinakamilisha mazoezi rasmi hii leo chini ya kocha mkuu Benni McCarthy. Mchezo huo wa Ijumaa utachezwa katika uwanja wa Orlando Stadium saa moja jioni kabla ya marudiano uwanjani Nyayo wiki ijayo. Kikosi cha Stars kimepata nguvu kufuatia kurejea kwa nahodha Michael Olunga na beki Eric Marcelo Ouma, ambao walikosa mechi zilizopita.