Huenda Seneta Omtata akajiunga na mrengo wa upinzani

  • | Citizen TV
    293 views

    Jopokazi lililoundwa la kukusanya maoni kuhusu azma ya Okiya Omtata ya kuwania urais linasema huenda Seneta huyo akajiunga na wanasiasa wengine wa upinzani kuunda mrengo utakaotimua rais William Ruto ofisini kwenye uchaguzi wa 2027. Mwenyekiti wa jopokazi hilo Mary Kathambi anasema kamati yake inakusanya maoni yatakazomwezesha Seneta huyo kufanya uamuzi na kutathmini kundi lipi la wanasiasa wenye azma sawia atakalojiunga nalo. Kwenye kikao kilichofanyika mjini Garissa, wakazi walisema wamechoshwa na viongozi wanaochaguliwa na kukosa kutekeleza wajibu wao.