Idara ya mahakama yapanga kuanzisha mahakama za zamu zitakazohudumu saa ishirini na nne

  • | K24 Video
    42 views

    Idara ya mahakama inapanga kuanzisha mahakama za zamu zitakazohudumu saa ishirini na nne kila siku ili kushughulikia kesi za dharura. Jaji mkuu martha koome amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa miaka 10 wa mabadiliko ya kijamii kupitia upatikanaji wa haki. koome pia amesema kuna haja ya kuwezesha mhimili huo wa serikali zaidi ili kufanikisha baadhi ya majukumu yake yanayolemazwa na changamoto za kifedha. Hafla hiyo ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na mkuu wa mawaziri musalia mudavadi ambaye amesisitiza haja ya kubuni sheria itakayosimamia mpito wa mamlaka baada ya uchaguzi