IEBC yafanya mkutano na wawaniaji urais

  • | K24 Video
    87 views

    Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imeagiza wawaniaji wote wa urais kuwasilisha angalau saini elfu 48 za wafuasi wao kufikia tarehe 25 mei la sivyo waondolewe kwenye kinyanganyiro, baadhi ya wawaniaji wakujitegemea wakidai kuwa masharti waliowekewa na IEBC ni magumu kuyatimiza. kinara wa Azimio Raila Odinga na naibu rais William Ruto hata hivyo hawakuhudhuria kikao hicho japo walituma wawakilishi wao. aidha, IEBC imesisitiza walioshtakiwa na kupatikana na hatia mahakamani hawataruhusiwa kugombea nyadhifa zozote katika uchaguzi wa Agosti.