- 5,927 viewsDuration: 3:54Tume ya uchaguzi nchini IEBC imemtoza faini ya shilingi milioni mbili unusu Mbunge wa Nakuru Town East David Gikaria kwa hatia ya kuwahonga wapiga kura kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa eneobunge la Ol Kalou alhamisi. IEBC inasema ina ushahidi wa kutosha kuwa mbunge huyo ana hatia. Haya yamejiri huku IEBC pia ikiwaonya wanasiasa na hata wakazi wa Ol Kaloo kudumisha amani kwenye uchaguzi huo, huku idara ya polisi ikisema maafisa elfu moja wametumwa kulinda usalama,