Imani ya wafuasi wa Kenya Kwanza kuhusu uongozi wa serikali ya muungano huo inafifia

  • | K24 Video
    44 views

    Imani ya wafuasi wa Kenya Kwanza kuhusu uongozi wa serikali ya muungano huo inafifia. Hii ni kulingana na matokeo ya utafiti wa kampuni ya TIFA yanayoonyesha imani hiyo imepungua kwa asilimia 12 kati ya mwezi machi na sasa. Ongezeko la gharama ya maisha ni miongoni mwa sababu kuu ambazo zinafanya asilimia kubwa ya wakenya kuona taifa linaelekea pabaya.