Iran yashambulia kwa mabomu kambi ya jeshi ya Doha

  • | BBC Swahili
    10,717 views
    Iran imezindua makombora dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Qatar na Iraq kufuatia mashambulizi dhidi ya maeneo yake ya nyuklia siku ya Jumamosi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran. Qatar imethibitisha shambulio hilo kwenye kambi ya Marekani ya Al Udeid, ikilieleza kama "ukiukaji wa wazi" na kusema ina haki ya kujibu moja kwa moja. Nchi hiyo pia imefunga kwa muda anga yake, na raia wa Marekani na Uingereza wameelekezwa kubaki ndani kwa usalama wao. - - #bbcswahili #iran #marekani #Israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw