Jaji: Makato ya 2.75% ni kutoza ushuru maradufu

  • | Citizen TV
    2,394 views

    Serikali imepata pigo baada ya mahakama kuu leo kuamua kwamba makato ya asilimia 2.75% ya bima ya afya ya SHIF kwenye mshahara si halali. Mahakama ikisema makato hayo ni sawa na kulipa ushuru mara mbili kwa mwajiriwa ambaye tayari anakatwa ushuru wa mapato. Haya yanajiri huku sha ikisema huenda ikashindwa kutoa hudumu za afya kwa baadhi ya wafanyakazi ambao waajiri wao hawafikishi malipo yao.